Taarifa za Sauti za Afya ya Mama na Mtoto
Ili kusikiliza toleo la sauti la taarifa hii kwa Kiswahili, bonyeza kitufe cha kucheza kilicho hapa chini.
Tafadhali hakikisha sauti yako iko juu. Inashauriwa kutumia vipokea sauti vya masikioni katika maeneo ya umma.
Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto ni huduma ya bure kwa wazazi na watoato wao wenye Umri wa kuanzia miaka sufuri hadi sita. Wakati mwangine huduma hii huitwa MCH.
Huduma ya MCH ni huduma muhimu na itakupatia wewe na mutoto wako taarifa muhimu kuhusu afya na maendeleo ya mutoto.
Muuguzi wa afya ya mama na mutoto atakuona wewe na mtoto wako katika kila miadi.Atapima Uzito na urefu wa Mtoto wako,na ata zungumuza nawe kuhusu ratiba za usingizi wa mutoto wako,malisho,chanjo na michezo. Anaweza pia kukuambia kuhusu huduma au mipangilio nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo,kama vile vikundi vya kucheza na chekechea. Muuguzi wa MCH yuko hapo kuku Saidia wewe na mutoto wako,na kujibu maswali yoyote uliyo nayo,hawako hapo kwa ajili yaku kuhukumu.
MCH (Huduma ya Afia ya mama na Mutoto)ni tofauti na Kwenda kwa daktari.Unaenda kwa Daktari ikiwa wewe au mtoto wako ni mugonjwa. Huduma ya MCH ni kwa ajili ya wototo walio na afya njema,na hutoa taarifa kwa wazazi ili kuwasaidia katika kukomaa na ustawi wa Watoto wetu.
Kuna ziara maalumu za MCH ambazo wewe na mtoto wako mnapaswa kuhudhuria. Ziara ya kwamza hufanyika nyumbanimuda mfupi baada yam toto wako kuzaliwa.Ziara zingine hufanyika mtoto wako anapofika umri Ufuatao:
Muuguzi wa Afya ya Mama na Mtoto anaweza.
Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto (MCH) itaandaa mkalimani kwa ajili ya miadi yako ikiwa utamhitaji. Huduma hii ni ya bure.
Kuhudhuria huduma ya Afya ya Mama na Mtoto pamoja na mtoto wako ni muhimu sana na itasaidia kuhakikisha mtoto wako anakua, anaendelea na kujifunza ipasavyo.
Ili kuweka miadi ya huduma ya Afya ya Mama na Mtoto, tafadhali piga simu 5832 9312.